Ushauri wa Kisheria (Legal Advisory)
BE Ako Law hutoa ushauri wa kitaalamu kwa masuala ya biashara, ajira, ardhi, ndoa, ushuru, na masuala ya kimataifa ya kisheria. Ushauri huu huwasaidia wateja kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuchukua hatua muhimu.
Uwawakilishi Mahakamani (Litigation Services)
Wanawakilisha wateja kwenye kesi mbalimbali mahakamani — ikiwemo migogoro ya mikataba, kazi, mirathi, bima, na uhalifu wa kiuchumi.
Mikataba na Nyaraka za Kisheria (Contracts & Legal Documentation)
BE Ako Law huandaa, hupitia, na kutoa ushauri kuhusu mikataba ya kibiashara, mikataba ya ajira, makubaliano ya ushirikiano na nyaraka nyinginezo za kisheria.
Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro (Arbitration & Mediation)
Kampuni inasaidia kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi na upatanishi ili kuepusha muda na gharama za kesi mahakamani
Sheria za Makampuni (Corporate & Commercial Law)
Wanatoa huduma kwa makampuni kuanzia usajili, mabadiliko ya kiutawala, compliance na kuandaa nyaraka muhimu za kampuni kama vile katiba na sera za ndani.
Sheria ya Mali Miliki (Intellectual Property Law)
BE Ako Law huwasaidia wateja kusajili, kulinda na kusimamia hakimiliki, chapa za biashara (trademark), na hata hataza (patents)
Kua wa kwanza Kutoa Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika Maoni YakoB&E Ako Law
BE Ako Law ni kampuni ya sheria (law firm) inayotoa huduma za kisheria kwa watu binafsi, wafanyabiashara, mashirika ya ndani na ya kimataifa. Kampuni hii inajivunia kuwa na timu ya wanasheria waliobobea katika nyanja mbalimbali, wakitoa huduma kwa weledi, uaminifu na kwa kuzingatia matakwa ya wateja wake.
Tovuti
https://beakolaw.co.tz
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 222771145