Huduma za Msaada wa Kisheria (Legal Aid Services)
TAWLA hutoa msaada wa kisheria bure kwa wanawake na watoto wanaokumbwa na changamoto kama vile: Migogoro ya ndoa na talaka Madai ya matunzo ya watoto Mizozo ya mirathi na umiliki wa mali
Ushauri wa Kisheria na Uwawakilishi Mahakamani
Wanatoa ushauri wa kisheria kwa wanaohitaji msaada wa kuelewa haki zao, na pia huwawakilisha mahakamani hasa wale wasioweza kumudu gharama za mawakili.
Elimu kwa Umma (Legal Education & Awareness Campaigns)
TAWLA huendesha semina, midahalo, na kampeni mbalimbali za uelimishaji kwa jamii juu ya haki za binadamu, usawa wa kijinsia, na sheria zinazolinda haki za wanawake na watoto.
Utafiti na Sera (Research & Policy Advocacy)
Chama hiki hufanya tafiti kuhusu hali ya haki za wanawake na watoto nchini, na kutumia matokeo hayo kushawishi maboresho ya sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia.
Uwezeshaji wa Wanawake (Women Empowerment Initiatives)
TAWLA hushirikiana na mashirika mengine kuendesha miradi ya kuwawezesha wanawake kiuchumi, kijamii na kisheria ili waweze kutetea haki zao
Mafunzo kwa Wanasheria na Watoa Huduma
Hutoa mafunzo maalum kwa wanasheria, watendaji wa serikali, na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuboresha utoaji wa huduma za haki kwa wanawake na watoto.
Kua wa kwanza Kutoa Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika Maoni YakoTanzania Womens Lawyer Association
Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) ni chama cha wanasheria wanawake nchini Tanzania kilichoanzishwa mwaka 1989. Kimejikita katika kulinda na kutetea haki za wanawake, watoto, na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu kupitia huduma za kisheria, elimu ya sheria kwa jamii, na ushawishi wa sera.
Tovuti
https://www.tawla.or.tz
Barua pepe
info@tawla.or.tz
Simu
+255 800751010