Chipsi Zege
Inatolewa na Sele Bonge Chipsi
Chipsi zege ni mchanganyiko wa mayai na chipsi unaopendwa sana katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Viazi hukaangwa kisha kuchanganywa moja kwa moja na mayai Ni mlo rahisi, wenye kushibisha, na hupatikana kwa wingi kwenye migahawa ya vyakula vya haraka (fast food) au vioski vya mtaani. Wengine hupendelea kuila ikiwa imeambatana na kachumbari au pilipili ya asili.