Huduma ya Dharura na Usafiri wa Wagonjwa
Inatolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Kuna kitengo cha dharura kinachopokea wagonjwa saa 24. Wagonjwa wanaopata ajali, hali za kupoteza fahamu, au magonjwa ya ghafla hupokelewa na kutathminiwa haraka. Pia kuna huduma ya ambulansi kwa wagonjwa wanaohamishwa kutoka au kuletwa hospitalini.