vifurushi vya post paid bando/biashara
Yas/tigo inakupatia Kifurushi cha POSTPAID/lipa baada ya matumizi. Ni huduma ya vifurushi vya malipo ya baada ambapo mtumiaji hulipa huduma baada ya kutumia, badala ya kulipa kabla kama katika huduma za prepaid bundle . Hii mara nyingi inajumuisha muda wa maongezi, ujumbe mfupi (SMS), na matumizi ya data kwa kipindi cha mwezi mmoja. Huduma hii inalenga zaidi kwa watumiaji wanaohitaji matumizi mengi ya mawasiliano na wanapendelea kulipa kwa kipindi cha baadaye badala ya kabla. Piga *147*00#
bando za Muda wa maongezi na GB zaidi
DAKIKA ZA MITANDAO YOTE: Furahia vifurushi vya Wiki vya #UjanjaNi kutoka Tigo. Jiachie kupiga simu bila kizuizi ukiwa dakika kibao za mitandao yote pamoja GB kibao kwa wiki nzima! Piga *147*00# chagua wiki kisha combo.
Bando za sms siku 30
Pata kifurushi bomba cha mwezi mzima kwa bei poa tu, kuchati na wateja wako au ndugu jamaa na marafiki zako.
Vifurushi vya Chuo
Jisajili katika Gazebo la Yas ndani ya chuo au karibu na chuo kilichoko karibu yako kujipatia ofa mbalimbali za bando kama Nametune,Kabang ndefu, Bila ku exipire na 300tshs bure. Kujiunga piga *148*00#.
Mnunulie Rafiki
Extender/Kifurushi cha kudumu. Kifurushi cha combo,Kifurushi Sauti,Kifurushi cha Interneti.Bidhaa zote hizi unazipata kwenye mtandao wa Yas mwezi mzima. Piga *147*00#
Huduma kwa wateja mix by yas
Huduma zipatikanazo kwenye huduma kwa Wateja namba 100. Ni kama zifuatazo: Kuzuia fedha zilizotumwa kimakosa,Kufunga akaunti ya Yas,mpangilio wa internet na nyingine kemkem.
Huduma ya Tigopesa/Mix by yas
Tigo/Yas ni kampuni inayotoa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya simu na kupitia programu elekezi Tigopesa app) na kusaidia mamilioni ya Watanzania kulipa kwa njia ya simu na kuendelea na maisha. Tigopesa/Mixx by YAS imekuwa mkombozi mkubwa wa huduma za kifedha nchini hususani kwa watu wa vijijini kwani inafanya kazi kama benki watumiaji wa huduma hiyo huhifadhi fedha kwenye simu zao na kutoa fedha kupitia wakala. Endelea kufurahia huduma za Tigo Pesa na kutuma pesa bure kwa wateja wa Tigo pesa nchi nzima kwa kupiga *150*01# au kupitia App yetu ya Tigo Pesa.
Hudumma za Mikopo ya fedha,Nivushe plus
Tigo sasa ni Yas na Tigo pesa ni Mixx by Yas. Tunawaunganisha Watanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali ili waweze kutimiza ndoto zao.Usikae kinyonge jipatie huduma ya mikopo ya muda wa maongezi,sms,na mtandaoni.
Andika Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika maoniMtandao Tigo/YAS
YAS ni kampuni ya mtandao wa huduma za simu awali ilijulikana kwa chapa ya Tigo. Chapa ya YAS imeziduliwa rasmi tarehe 26 Novemba 2024. Kampuni hiyo wakati inaingia nchini Tanzania miaka takribani 30 iliopita ilianza kwa jina la Mobitel kabla ya kuitwa Tigo. Pia YAS imetangaza mabadiliko ya jina kwenye bidhaa yake ya TIGO PESA ambayo kuanzia leo itakuwa ikiitwa MIXX BY YAS. Hii sio mara ya kwanza kwa Kampuni hii kubadilishwa jina ilikuwa Mobitel (BUZZ), kisha TIGO na sasa ni YAS! Mabadiliko haya yametangazwa na Uongozi wa Kampuni hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo mchana ambayo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa.
Tovuti
http://www.tigo.co.tz
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 713123103