Ushauri wa Kisheria (Legal Advisory Services)
Wanatoa ushauri wa kisheria katika nyanja tofauti kama vile sheria za ardhi, ndoa, mirathi, biashara, ajira, na mali miliki. Hii huwasaidia wateja kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kisheria.
Uandishi na Mapitio ya Mikataba (Contract Drafting & Review)
AK Tanzania huandaa na kupitia mikataba ya kibiashara, ya kazi, au makubaliano mengine ili kuhakikisha inalinda maslahi ya wateja wao.
Uwawakilishi Mahakamani (Litigation)
Wanatoa uwakilishi kwenye mahakama mbalimbali kwa wateja wenye kesi za madai, migogoro ya ardhi, migogoro ya kibiashara, migogoro ya kifamilia, na nyinginezo
Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro (Dispute Resolution & Mediation)
Kwa wale wanaotaka kuepuka mchakato wa mahakama, AK Tanzania huwasaidia kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi na upatanishi kwa lengo la kupata suluhu ya haraka na yenye tija.
Huduma za Sheria za Makampuni (Corporate Legal Services)
Wanashughulika na usajili wa makampuni, masuala ya utawala wa kampuni, compliance, na masuala mengine ya kisheria yanayohusu uendeshaji wa biashara.
Huduma za Mirathi na Nyaraka za Kisheria (Probate & Notarial Services)
Wanasaidia wateja katika kushughulikia mirathi, maandalizi ya wasia, na nyaraka muhimu kama vile hati ya udhamini, mkataba wa ndoa, na uthibitisho wa nyaraka (notarization)
Kua wa kwanza Kutoa Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika Maoni YakoA&K Tanzania
AK Tanzania ni kampuni inayotoa huduma za kisheria kwa weledi na uwajibikaji mkubwa. Ikiwa ni miongoni mwa watoa huduma katika sekta ya sheria nchini, AK Tanzania inahudumia wateja wa aina mbalimbali — watu binafsi, makampuni, wawekezaji na mashirika — kwa kuhakikisha wanapata ulinzi wa kisheria na mwongozo sahihi katika shughuli zao.
Tovuti
https://aln.africa
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 754999667