Ununio Beach Park/Fukwe
Fukwe hii inapatikana Ununio, jijini Dar Es Salaam mita chache kutoka kituo cha daladala cha Ununio Sifa kuu ya fukwe hii ni mazingira masafi kwenye maeneo mengi ya wazi yanayotumiwa kwa kupumzika, burudani na michezo mbalimbali kama mpira na bembea kwa watoto Eneo hilo lina migahawa yenye vyakula mbalimbali ikiwemo vyakula vya baharini (sea foods), burudani ya muziki kutoka kwa Dj’s au bendi zinazokuja kutumbuiza kwa ratiba walizojiwekea. Kama unapenda huduma za ‘kishua’ yaani huduma za hadhi za juu, kwenye fukwe huyo pia kuna hoteli jirani ambayo pia hauhitaji kiingilio ila utalazimika kununua na vinywaji kutoka hapo. Karibu Ununio Beach Park kufurahi pamoja na familia yako! Hapa, furaha ni bure kabisa! Jiunge na shangwe, michezo, na burudani tele bila malipo
Tovuti
ununiobeachpark.co.tz
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 757733378