National Benki of Commerce (Tanzania) NBC-Benki
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usimamizi mzuri wa fedha. Historia ya Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaani mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya Biashara, iligawanywa katika tanzu tatu tofauti: NBC Holding Corporation National Microfinance Bank (NMB) NBC (1997) Limited Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), lilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.
Tovuti
https://www.nbc.co.tz
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 222199793